Jumatatu 14 Aprili 2025 - 20:29
Utata katika mwenendo wa Marekani ndio chanzo cha vita sehemu mbali mbali

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika taarifa kuhusu mazungumzo yake kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani, amesisitiza kuwa: Mazungumzo haya yanaweza tu kuzaa matokeo chanya na ya kudumu ikiwa yatafanyika katika mazingira yanayozingatia msingi wa usawa, kuheshimiana, na mbali na vitisho au mashinikizo yoyote ya kisiasa.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Shura ya maulamaa wa Kishia Pakistan, katika taarifa yake kuhusiana na mazungumzo yanayo endelea kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani, amesisitiza kuwa: Mazungumzo haya yanaweza tu kuwa na matokeo chanya na ya kudumu ikiwa yatafanyika katika mazingira yanayozingatia msingi wa usawa, kuheshimiana, na mbali na vitisho au mashinikizo yoyote ya kisiasa.

Akiwakosoa maafisa wa Marekani kwa matamshi yao ya vitisho kabla ya kuanza kwa mazungumzo, alieleza kwa uwazi kuwa: Kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran ni mfano wa wazi wa kukiuka mamlaka ya kitaifa ya nchi huru, na jamii ya kimataifa inapaswa kutoa msimamo madhubuti na kuwajibika dhidi ya mitazamo hatarishi na ya uchochezi kama hiyo.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistani aliongeza kuwa: Uzoefu wa kihistoria unaonesha kwamba makubaliano ya kudumu na yenye manufaa hupatikana pale ambapo pande mhusika huingia katika mazungumzo kwa misingi ya maslahi ya pamoja, kuaminiana na kuheshimu misingi ya kimataifa, na si kwa mtazamo wa kujiona bora au kutaka kutawala. Mwenendo wa upande mmoja wa Marekani si tu kwamba unahujumu amani ya dunia, bali pia unaandaa mazingira ya kuzidisha migogoro sehemu mbali mbali.

Rais wa Shura ya wanazuoni wa Kishia Pakistan, akizungumzia sera za kinafiki za Marekani na utawala wa Kizayuni, alieleza kuwa: Wakati ambapo Magharibi inajitahidi kuizuia Iran kufikia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani, wakati huohuo inataka nchi za kiislamu kama vile Pakistan, zilikubali kuwepo kwa utawala wa Kizayuni. Utata huu wa wazi umeufichua sura halisi ya wale wanaojidai kuwa watetezi wa demokrasia na haki za binadamu duniani.

Aidha, alitaja pia athari mbaya za uungaji mkono usio na masharti wa Marekani kwa utawala wa kigaidi wa Kizayuni, na kusisitiza kuwa: Sera hizi ndizo chanzo kikuu cha migogoro na vita maeneo mbalimbali, na kuendelea kwake kunaweza kuusukuma ulimwengu kuelekea katika mizozo mipana zaidi.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, kwenye hitimisho lake, alielezea matumaini yake kuwa mazungumzo kati ya Iran na Marekani yatamaliza hali ya uhasama wa kimazingira, yataimarisha nafasi ya uhuru wa Iran, na kuwa hatua muhimu kuelekea katika kutimia kwa amani na utulivu wa kudumu maeneo mbali mbali na duniani kwa jumla.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha